Jumanne , 10th Jan , 2017

Shirikisho la Soka Duniani FIFA limepitisha mabadiliko ambapo kuanzia mwaka 2016 timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia zitaongezeka kutoka 32 hadi 48.

Kombe la Dunia, litaongezeka kwa kuwa na timu shiriki 48, kutoka 32 sasa, baada ya kikao cha Shirikisho la Soka Duniani FIFA, kupitisha maamuzi hayo, mjini Zurich, Uswiss, hii leo.

Jumla ya makundi 16, ya timu tatu kila, moja, yatacheza hatua ya makundi na washindi wawili wa kila kundi wataingia hatua ya mtoano kwa timu 32.

Ongezeko la timu kwenye kombe la dunia, utaanza kutumika kwenye fainali za mwaka 2026, huku kukiwa kuna uwezekano mkubwa kwa Afrika kupewa nafasi tisa badala ya tano za sasa.

Idadi ya mechi zitakazo pigwa ni 80, kutoka 64 za sasa, lakini washindi wataendelea kucheza mechi 7 tu, kama ilivyo sasa.