Jumatano , 25th Mei , 2022

Mcheza tenisi namba moja Uingereza kwa wanawake Emma Raducanu ametolewa kwenye michuano ya wazi ya Ufaransa (French Open) raundi ya pili ya michuano kwa kufungwa kwa seti 2-1 na Aleksandra Sasnovich.

Emma Raducanu

Raducanu mwenye umri wa miaka 19 alianza vyema katika mchezo huo kwa kushinda seti ya kwanza kwa 6-3 na alionekana kuumudu mchezo lakini Aliaksandra alirejea na kushinda seti ya pili na ya tatu kwa 6-1, 61 na kufuzu raundi inayofata kwa ushindi wa seti 2-1.

Umekuwa mwaka mbaya kwa Emma ambaye ameshinda michezo miwili tu ya Grand Slam mwaka 2022, na amekuwa na changamoto ya kuwa na muangalizi kwenye eneo la kocha wa kumnoa na kabla ya kuanza kwa michuano hii aliachana na kocha wake Torben Beltz.

Aleksandra Sasnovich raia wa Belarus baada ya kumtoa Raducanu katika hatua inayofata, raundi ya tatu atacheza dhidi ya mjerumani Angelique Kerber.