Jumatatu , 19th Apr , 2021

Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema kuwa presha ni sehemu ya mchezo wa mpira wa miguu jambo ambalo hana hofu nalo katika historia yake.

Kiungo na nahodha msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima akizungumza na Waandishi wa Habari.

Kiungo huyo mwenye uwezo wa kuuchezea mpira na ukamtii kwa sasa anapambania malengo ya timu yake hiyo inayohitaji kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ulio mikononi mwa Simba.

Kesho ina Yanga iliyo nafasi ya Kwanza na pointi 54 ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Gwambina FC iliyo nafasi ya 12 na pointi 30.

Niyonzima amesema:" Tangu nije Tanzania Yanga haijawahi kukosa ubingwa mara tatu mfululizo kama ilivyokuwa kwa sasa na ninaweza kusema kwamba hiki pia kimechangia presha.

"Mimi sijawahi pats presha ya namna hiyo kwa kuwa presha ipo siku zote lakini jambo la kawaida katika mpira na mimi ninapenda kuwaambia wachezaji kuwa mchezaji yoyote ambaye hakubali presha bora aache mpira,".