Jumatano , 27th Jan , 2021

Timu ya taifa ya Tanzania taifa stars itajua hatma yake ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano ya CHAN leo saa 4:00 Usiku, ambapo itashuka dimbani dhidi ya timu ya taifa ya Guinea kwenye mchezo wa mwisho wa kundi D,Taifa stars inahitahi ushindi ilikusonga mbele.

Kikosi cha timu ya Taifa “Taifa Stars” wakiwa kwenye mazoezi Uwanja wa Bonamoussadi,Douala kuelekea mchezo wa mwisho Kundi D mashindano ya CHAN vs Guinea leo.

Timu hizi zinatofautiana alama 1 tu kwenye msimamo wa kundi D, Guinea ndio vinara wa kundi wakiwa na alama 4, baada ya kuifunga Namibia mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 Zambia kwenye mchezo uliopitana, wakati Tanzania wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 3 alama ambazo walizipata kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namibia baada ya kupoteza mchezo wa kwanza mbele ya Zambia.

Timu itakayoshinda mchezo huu itafuzu kucheza hatua ya robo fainali, lakini matokeo ya sare yatakuwa na faida zaidi kwa Guinea, matokeao pekee yatayaoivusha taifa stars ni matokeo ya ushindi tu pasipokujalisha matokeo ya mchezo mwingine wa kundi hili ambao unazikutanisha Namibia ambayo inaburuza mkia kwenye kundi ikiwa haina alama hata moja na Zambia ambao wana alama 4 wakiwa nafasi ya pili mchezo ambao utachezwa Saa 4:00 Usiku.

Mshindi wa kundi hili atacheza na mshindi wa pili wa kundi C’ timu ya taifa ya Rwanda na timu itakayomaliza nafasi ya pili kwenye kundi D itacheza na kinara wa kundi C ambao ni mabingwa watetezi timu ya taifa ya Morocco.