Ni ngumu kuitoa Chelsea kileleni - Guardiola

Tuesday , 14th Feb , 2017

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema pengo la pointi kati yao na Chelsea, ni kubwa sana licha ya kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Bournemouth katika Uwanja wa Vitality, na kukwea hadi nafasi ya pili.

Pep Guardiola (kushoto) na kocha wa Bournemouth baada ya mechi ya jana

Huku timu hizo zikitofautiana pointi 8, Guardiola amesema ni vigumu kwa Chelsea kupoteza michezo yake na wao kushinda kila mechi kama ilivyoteka jana. 

"Pengo bado refu sana, kwa hiyo huwezi kuwatarajia (Chelsea) kupoteza michezo, na vilevile ni vigumu kushinda michezo yote". Guardiola alisema.

Mshambuliaji wa Manchester City Muargentina Sergio Aguero alianza mechi hiyo akiwa benchi lakini alichukua nafasi ya Mbrazili Gabriel Jesus baada ya dakika 14 tu kufuatia Mbrazili huyo kupata jeraha.

Mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling alifunga goli la ufunguzi katika dakika ya 30, huku goli la pili la City lilikuwa la kujifunga kupitia Tyrone Mings katika dakika ya 69.

Recent Posts

Mch. Anthony Lusekelo

Current Affairs
Mzee wa Upako afunguka kuhusu yeye kunywa pombe

Shamba la bangi tayari kwa kuteketezwa, huku mtuhumiwa wa kilimo hicho akiwa chini ya ulinzi (Picha: Maktaba)

Current Affairs
Ukikutwa na shamba la bangi, jela miaka 30

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiambatana na Waziri Charles Mwijage kukagua eneo ambapo kitajengwa kiwanda cha vigae.

Current Affairs
Kikwete 'alivyopora dili' la kiwanda cha vigae