Jumamosi , 19th Aug , 2017

Klabu ya Barcelona imemsajili kiungo Mbrazil Paulinho kutoka katika timu ya Guangzhou Evergrande ya China kwa dau la pauni milioni 36.4.

Paulinho

Mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham (29) amekuwa ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu hiyo ya Hispania tangu Neymar alipoondoka na kujiunga na Paris St-Germain kwa uhamisho ulioweka rekodi.

Paulinho alijiunga na Tottenham kwa dau la pauni milioni 17 akitokea Corinthians mwaka 2013, kabla ya kuhamia China 2015.

Paulinho alisema: "Unatakiwa kukabiliana na changamoto kwa kujiamini. Nitajaribu kufanya kazi yangu vizuri na nimejiandaa kwa hilo.Ni wakati sahihi kwangu. Ndoto ambayo niliitarajia sasa imetimia. Nitawafanyia kila kitu."

Barcelona pia inaendelea na mchakato wa kupata saini ya kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho pamoja na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele.