Ndikumana ambaye pia ni baba wa watoto wawili huku mmoja akiwa amezaa na Irene Uwoya, amezikwa na mamia ya wadau wa soka nchini humo wakiwemo mashabiki wa klabu ya Rayon Sport, ambayo alikuwa akifanyia kazi kama kocha msaidizi.
Taarifa zaidi zinasema kwamba Irene Uwoya hakuwahi kuhudhuria mazishi hayo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.
Ndikumana alifariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake nchini Rwanda, na kuacha majonzi makubwa kwa wapenzi wa soka na watu wake wa karibu, kutokana na kifo chake kilichotokea ghafla bila kuumwa.
Tazama hapa watu walivyojazana msibani