Jumatatu , 28th Sep , 2020

Timu ya Taifa ya Tanzania' Taifa Stars' itacheza mechi ya kirafiki katika Kalenda ya FIFA ya Burundi, Oktoba 11, 2020 Saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije akitoa maelekezo.

Kocha mkuu wa Taida Stars, Etienne Ndayiragije atatangaza kikosi Oktoba 2, 2020.

Taifa Stars inajiwinda na mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia la 2022, Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) na Fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani .