Jumamosi , 18th Nov , 2017

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema mshambuliaji wa timu hiyo Zlatan Ibrahimovic ataanzia benchi kwenye michezo yake ya mwanzo ili aendelee kuimarika zaidi.

Ibrahimovic leo anatarajiwa kurejea dimbani baada ya kukosekana kwa muda mrefu kutokana na maumivu ya goti yaliyomweka nje kwa kipindi kirefu. 

“Atakuwa anaanzia benchi kwa mechi za mwanzo ili aweze kurejea vizuri, lakini uhakika ni kuwa amepona na tupo naye kwenye kikosi chetu kwaajili ya kuongeza ushindani”, amesema Mourinho.

Kwa kauli hiyo ya Mourinho inaashiria kuwa Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 36, atacheza dakika chache kwenye mchezo wa leo dhidi ya Newcastle. Manchester United leo inawakaribisha pia nyota wake Paul Pogba na Marcos Rojo ambao walikuwa majeruhi kwa kipindi kirefu.

Kwa upande wa nafasi ya Ibrahimovic mbele ya Lukaku Mourinho amesema kuwa ataendelea na mfumo wa kuchezesha washambuliaji wawili hivyo watakuwa wanacheza pamoja au kupishana pale inapobidi au itategemeana na mazinbgira ya mchezo husika.