Jumamosi , 28th Nov , 2020

Klabu ya Namungo ambayo ni miongoni mwa klabu wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Afrika, inataraji kushuka dimbani saa moja usiku wa hii leo kwenye dimba la chamazi temeke Dar es salaam kuvaana na klabu ya Al Rabita kutoka Sudan Kusini kwenye kombe la shirikisho Afrika.

Kikosi cha Namungo FC

Kuelekea kwenye mchezo huo ambao ni wa hatua ya awali ya mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika, Afisa Habari wa Namungo Chindamba Namlia amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na dhamira yao ni kupata ushindi nyumbani.

Maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Al Rabita yamekamilika, wachezaji wako kwenye hali nzuri, morali ipo juu. Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda nyumbani ili iwe rahisi kwenye mechi ya marudiano ugenini”. Kindamba Namlia, Msemaji wa Namungo FC.

Kwa Upande wa kocha wa Namungo, Hemed Suleiman 'Morocco' amesema licha ya kukosa CD za kumsaidia kumuoneshea video za marudio ni namna gani wapinzani wake wanacheza ili iwe rahisi kuwakabiri, amesema bado anaamini maandalizi yao yatawasaidia kufanya vizuri kwenye mchezo huo.