Jumanne , 19th Jul , 2022

Timu ya taifa ya Afrika kusini wamepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Zambia na kutinga hatua ya fainali ya michuano ya mataifa huru ya Afrika ya Wanawake 'WAFCON' kwa goli liliofungwa na Linda Motlhalo kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 90.

Wenyeji wa michuano ya WAFCON 2022 timu ya taifa ya wanawake ya Morocco

Kwenye nusu fainali ya pili, wenyeji Morocco nao walifanikiwa kutinga fainali baada ya kuwalaza Nigeria kwa mikwaju ya penati 5 kwa 4 baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Nigeria walikua wa kwanza kupata goli baada ya Yasmin Mrabet wa Morocco kujifunga katika dakika ya 62, goli liliodumu kwa dakika 4 tu kabla ya Morocco kusawazisha kupitia kwa Sanaa Mssoudy katika dakika ya 66.

Sasa Zambia na Nigeria zitapambana katika mchezo wa kuwania nafasi ya mshindi wa tatu mchezo utakao pigwa ijumaa hii Julai 22, 2022 katika uwanja wa Mfalme Mohammed wa tano nchini Morocco majira ya saa 5:00 usiku.

Nao wenyeji Morocco wataumana na Africa ya kusini katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo mikubwa ya soka la wanawake barani Africa siku ya Jumamosi Julai 23, 2022 katika uwanja huo huo wa mfalme wa tano wa Morocco majira ya saa 5:00 usiku.