Jumamosi , 23rd Sep , 2017

Mshambuliaji mpya wa Chelsea Alvaro Morata aliyesajiliwa msimu huu akitokea Real Madrid amefunga 'hattrick' yake ya kwanza kwenye mchezo wa EPL dhidi ya Stoke City, na kuifanya timu hiyo kung'ara katika dimba la Selhurst Park nchini England.

Alvaro Morata

Morata alianza kuona lango la Stoke City kwenye dakika ya 2, kisha akaja kuingia nyavuni tena dakika ya 78, na ilipofika dakika ya 82 Morata aliandika historia yake ya kupiga 'hattrick' kwa kufunga goli la 3. 

Naye Pedro Rodriuez alimsaidia Morata kuongeza idadi ya mabao, kwa kuifungia timu yake ya Chelsea kwenye dakika ya 30 na kuifanya timu hiyo kutoka na mabao manne.

Timu ya Stoke City imetoka nunge na kuifanya kukosa point 3, ambazo iwapo wangezipata wangekuwa na point 8.

Kwa hattrick hiyo na namna ambavyo Morata amelisakata kabumbu leo, Morata ametajwa kuwa 'Man of the match' kwenye mechi hiyo ya EPL iliyochezwa leo.