Ijumaa , 17th Nov , 2017

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Azam FC Wazir Junior amefiwa na mama yake mzazi usiku wa kuamkia leo nyumbani kwao wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Taarifa kutoka klabu hiyo zimethibitisha msiba huo ambapo tayari mchezaji huyo amepewa ruhusa ya kwenda nyumbani kwaajili ya kushiriki msiba huo wa mama yake.

Klabu ya Azam FC imepokea kwa masikito makubwa msiba huo mzito wa mama yake Wazir hivyo imeungana na familia nzima kwenye kipindi hiki kigumu.

Wazir alikuwa amesafiri na timu kuelekea Njombe kwaajili ya mchezo wa ligi wikiendi hii dhidi ya Njombe Mji lakini tayari ameenza safari ya kurejea Dar es salaam asubuhi hii ambapo ataunganisha hadi Lushoto Tanga.

Uongozi wa Azam FC kwa niaba ya mashabiki na klabu kwa ujumla, umetoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na familia ya Junior.