Jumatatu , 13th Nov , 2017

Mshambuliaji wa zamani wa Argentina Gabriel Batistuta, amekiri kuwahi kuchukizwa na kitendo cha Messi kuvunja rekodi yake ya ufungaji wa mabao katika taifa hilo.

“Nilikasirika baada ya rekodi yangu ya mabao 54 kuvunjwa na Lionel Messi mwaka jana, lakini upande mwingine nilifurahi kwasababu ilivunjwa na mchezaji wa kiwango cha ajabu”, amesema Batistuta.

Batistuta ameongeza kuwa Messi ni mchezaji wa sayari nyingine lakini kitendo cha kuvunja rekodi yake kilimfanya ajisikie wivu kutokana na kwamba rekodi hiyo haikuwa imedumu sana.

Messi alivunja rekodi ya Batistuta ya mabao 54 kwenye timu ya taifa ya Argentina katika michuano ya Copa America Centenario mwaka jana ambapo hadi sasa ana jumla ya mabao 61 akiwa ndiye mfungaji bora wa muda wote.

Pamoja na hayo Batistuta amesema anajivunia kuwa mfungaji bora wa pili nyuma ya mchezaji ambaye si wa kiwango cha kawaida hivyo kwake ni kitu kizuri. Amemaliza kwa kusema sikuhizi watu hawaonyeshani tena kuwa yeye ndiye mfungaji bora wa Argentina.