Jumamosi , 19th Aug , 2017

Mchenga BBall Stars wamefanikiwa kuwachapa wapinzani wao TMT kwa pointi 87-82 mchezo wa tatu kati ya mitano katika fainali ya Sprite BBall Kings uliyopigwa katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Nahodha wa Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuph akimuwekea kizingiti mchezaji kutoka TMT, Erick Lugora.

Kutokana na matokeo hayo timu ya Mchenga BBall Stars imeweza kurudisha furaha kwa mashabiki zao baada ya kupoteza mechi iliyopita katika fainali hizi za Sprite BBall Kings kwa kuchapwa kwa pointi 87-78 na mpinzani wake TMT.

Pamoja na hayo, mechi ya leo iliweza kuonyesha utofauti mkubwa katika mechi zote zilizowahi kuchezwa katika michuano hii, kutokana na wachezaji wa pande zote mbili kuonyesha umahili wao waliyokuwa nao katika kucheza pamoja na kushambulia.

Mamia ya mashabiki waliyoweza kujitokeza kutazama mtanange wa fainali za Sprite BBall Kings leo Don Bosco Oysterbay 

Kwa upande mwingine, mchezaji Erick Lugora kutoka TMT ameweza kuibuka 'best scorer' kwa pointi 23 akifuatiwa na Marcelo Nyirabu kutoka Mchenga BBall Stars kwa kupata pointi 18 katika mechi ya tatu ya fainali za Sprite BBall Kings.

Mchenga na TMT zitakutana tena Agosti 23 (Jumatano) ya mwaka huu kucheza game 4 ambapo mchezo huo kwa upande mmoja utaweza kuwa wa mwisho endapo Mchenga BBall Stars akiweza kufunga tena.