Ijumaa , 13th Jan , 2017

Timu ya Mbeya city ya jijini imeahidi kudhibiti suala la uuzwaji holela wa jezi za timu hiyo , kutokana na kuwepo kwa watu ambao wanauza na kutengeneza jezi hizo bila kuwepo kwa makubaliano yoyote.

Mashabiki wa Mbeya City

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Timu hiyo, Emmauel Kimbe wakati wa kikao cha kujadili mustakabali wa soka, Mkoa wa Mbeya, ambapo amesema kuwepo kwa tabia hiyo kumekosesha mapato katika timu hiyo.

Aidha wadau wa soka mkoa wa Mbeya akiwemo Elizabet Mwanguku wameeleza masikitiko yao juu ya kushuka kwa viwango vya mpira kwa timu za Mbeya City na Prison, na kusisitiza kuundwa kwa Kikosi kazi kitakachoshughulikia masuala ya Soka.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, ambaye alikuwa Mwenyekiti katika kikao hicho amesema kuwa furaha yake ni kuona mkoa unaongeza timu nyingi zitakazoshiriki ligi kuu Tanzania bara.

Wasikilize hapa chini wakieleza undani wa hili...........................

 

Mdau Elizabet Mwanguku
Sauti ya Katibu Mkuu, Emmauel Kimbe
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla