Jumamosi , 25th Mar , 2017

Kocha wa timu ya Taifa ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" Salum Mayanga amewataka mashabiki kuonesha uzalendo kwa timu yao hii leo katika mchezo wa kirafiki ya kimataifa katika wiki ya kalenda ya FIFA didi ya Botswana utakaochezwa Uwanja wa Taifa

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga

Mayanga amesema, mashabiki ni sehemu ya timu na wana uwezo mkubwa wa kuhakikisha timu inafanya vizuri licha ya kiwango kizuri cha timu hiyo.

"Timu ipo katika kiwango kizuri na naamini leo watapambana ili kuhakikisha tunapata ushindi ambao utatusogeza katika nafasi nzuri lakini mashabiki nao wana uwezo mkubwa wa kuongezea ushindi katika mchezo huo, tunawaomba wajitokeze ili kuweza kuangalia kikosi chao kinavyofanya kazi," amesema.

Mbali ya mchezo huo hii leo, Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo mwingine dhidi ya Burundi Jumanne ijayo, Machi 28, mwaka huu, mchezo ambao pia ni wa kirafiki wa kimataifa.

Wachezaji Taifa Stars wakiwa mazoezini