Alhamisi , 9th Nov , 2017

Klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na mashabiki wake kurusha uwanjani chupa zinazosadikiwa kuwa na mikojo katika mchezo dhidi ya mahasimu wao Simba Sc katika dimba la Uhuru, October 28.

Adhabu hiyo imetolewa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kupitia ripoti za michezo yote ya Ligi Kuu, Daraja
la Kwanza na Daraja Pili.

Katika mechi hiyo iliyopigwa October 28 na kumalizika kwa sare ya 1-1, bao la Simba likifungwa na Shiza Kichuya na la Yanga likifungwa na Mambia, Obrey Chirwa, ,mashabiki wa Yanga walianzisha fujo kwa kutupa makopo yanayosemekana kuwa yalikuwa na mkojo na kuleta fujo

Mabingwa hao mara tatu mfululizo, wanatarajiwa kuteremka tena dimbani,Novemba 19 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kumenyana na Mbeya City.