Jumatano , 11th Jan , 2017

Siku moja mara baada ya Wekundu wa Msimbazi Simba kufanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi, baadhi ya mashabiki wa soka hapa nchini wamekuwa na maoni tofauti juu ya mchezo huo.

Baadhi ya wachezaji wa Simba wkishangilia ushindi wao hapo jana usiku.

Wakiongea na Hotmix Michezo hii leo mashabiki hao wamesema mchezo huo wa watani wa jadi ambao ulishuhudia Yanga wakifurushwa kwa mikwaju ya penalti 4-2 kufuatia sare tasa ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za mchezo huo uliofanyika jana usiku katika dimba la Amaan, visiwani Zanzibar kuwa ulikuwa mchezo uliotegemea bahati zaidi kutokana na timu zote kulingana kiuwezo.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao ni Tall Mrangi na Matipuli Sayona wakazi wa Jijini Dar es Salaam wamesema timu yao ilichezo vizuri lakini kilichowabeba Simba ni bahati katika hatua ya matuta.

Ikumbukwe kwa ushindi huo sasa Simba na Azam zitakutana tena katika fainali ya mashindano hayo siku ya Ijumaa Januari 13 mwaka huu ikiwa ni miaka mitano imepita tangu timu hizo zilipokutana katika nusu fainali mnamo mwaka 2012.