Jumanne , 26th Jan , 2021

Matajiri wa jiji la Manchester, klabu ya Manchester City itashika usukani wa ligi kuu nchini humo endapo ikifanikiwa kupata ushindi leo Januari 26, 2021saa 5:15 usiku itakapokuwa ugenini kucheza dhidi ya klabu ya West Bromwich Albion.

Wachezahi wa klabu ya Manchester City wakishangilia baada ya kupata bao.

Manchester City kwasasa ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 38 baada ya kucheza michezo 18 tofauti ya mchezo mmoja na alama mbili nyuma ya kinara wa ligi kuu nchini England, klabu ya Manchester United inayonolewa na kocha Ole Gunnar Solskjear.

City itajitupa dimbani kuwania alama tatu hizo muhimu bila ya nyota wake wawili tegemezi, kiungo Kevin De Bruyne mwenye maumivu ya nyama za paja na mshambuliaji wake Sergio Aguero anaeendelea kujitenga karantini baada ya kuwa na maambukizi ya Covid-19.

(Kiungo mshambuliaji wa Manchester City, Kevin De Bruyne atakayekosekana kutokana na majeraha )

(Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero ambaye pia atakosekana kutokana na kuwa karantini )

Kwa upande wa dimba la St.Mary’s, Klabu ya Southampton itawakaribisha washika mitutu wa jiji la London klabu ya Arsenal usiku wa leo bila ya kiungo wake mzoefu Oriol Romeu ilhali Arsenal ikiwa na mashaka kama nahodha wake Pierre Emerick Aubameyang atacheza.

(Mshambuliaji wa Arsenal, Pierre Emerik Aubameyang, mashakani kuukosa mchezo wa usiku wa leo )

Aubameyang alikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi kutokana na sababu binafsi hivyo mpaka sasa haijajulikana rasmi kama atakuwa tayari kuwavaa Southampton leo Januari 26, 2021 saa 5:15 usiku.

Arsenal ipo nafasi ya 11 wakiwa na alama 27 utofauti wa alama 7 na anayeshika nafasi ya nne klabu ya Liverpool ilhali Southampton ipo nafasi ya 10 wakiwa na alama 29, alama 2 mbele ya Arsenal.

Michezo miwili ya mapema ya EPL ni ile itakayopigwa saa 3:00 usiku wa leo, Crystal Palace dhidi ya Westham United wakati huo huo Newcastle United watacheza na Leeds United.