Jumapili , 23rd Apr , 2017

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia Haji Manara (Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba) kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na pia anatakiwa kulipa faini ya Shilingi  Milioni tisa.

Haji Manara

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Jerome Msemwa amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya Manara kukutwa na makosa matatu dhidi ya TFF ambao ni walalamikaji.

Makosa hayo ya Manara dhidi ya mlalamikaji TFF ni kuituhumu na kuidhalilisha TFF, kueneza chuki za ukabila na la tatu kuingilia utendaji wa shirikisho hilo.
Siku chache zilizopita  Manara aliituhumu TFF kufanya njama za waziwazi ili kuwabeba wapinzani wao Yanga kwenye Ligi Kuu.

Manara pia aliwatuhumu viongozi wakuu wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa ni wahaya na viongozi wa zamani wa Yanga, ambao wanataka kuipendelea Kagera Sugar.