Alhamisi , 21st Jul , 2022

Msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara amepewa adhabu ya kufungiwa miaka miwili leo Julai 21.

Haji Manara

Adhabu hiyo imetokana na makosa ambayo amekutwa nayo kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania.

Baada ya adhabu hiyo,Haji Manara ametoa kauli ya kwanza baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutojihusisha na soka kwa miaka miwili ameandika haya;

“Iwe ni jambo la kheri au shari, neno langu kuu ni kumshukuru muumba mbingu na ardhi kwa neno moja kubwa na lenye maana pana sana. AL-HAMDULILLAH,”