Hamiliton ameongoza mbio hizo mwanzoni kabisa baada ya Sebastian Vettel kugongana na dereva mwenzake wa Ferrari Kimi Raikkonen pamoja na Max Verstappen wa Red Bull na kumuacha Hamiliton akiongoza mbio hizo hadi mwisho.
Sebastian Vettel na wenzake walijitoa baada ya kugongana hivyo inawabidi wasubiri mbio zinazokuja ili kuona kama wanaweza kumpiku Hamiliton.
Mbio za leo za SingaporeGP zimefanyika usiku kwa mara ya kwanza katika historia ya Formula1. Lewis Hamiliton sasa amejiongezea pointi 25 ambazo zinamfanya kufikisha pointi 263 dhidi ya 235 za Sebastian Vettel.