Jumatatu , 18th Oct , 2021

Mshambuliaji nyota wa PSG, Kylian Mbappe amezidi kuwaacha wengi njia panda juu ya hatma yake mara baada ya kuweka picha yake na rais wa timu hiyo Nasser Al-Khelaifi kwenye Instagram akaunti yake na kuandika ujumbe wa shukrani.

Mshambuliaji nyota wa PSG, Kylian Mbappe.

Mbappe ameandika “Nina njaa ya mafanikio siku zote, Ahsante sana PSG” ujumbe ambao unatafsiri nyingi ikiwemo kuashiria amerejesha furaha yake klabu hapo hivyo huenda akassalia kwa kuongeza mkataba mpya.

(Kylian Mbappe akiwa ameshikilia tuzo na rais wa klabu hiyo, Nasser Al-Khelaifi ya mchezaji bora wa mchezo wa PSG 2-1 Angers)

Mbappe ameweka picha hiyo baada ya kuibuka kuwa nyota wa mchezo kwa kufunga bao moja na kutoa assist kwa Danilo Perreira kuisadia PSG kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuibakisha kileleni kwenye msimamo wa ligue 1.

PSG ina alama 27 kwenye michezo 10 iliyocheza, huku wakiwa wamepoteza mchezo mmoja pekee na kuiacha Lens kwa alama 9.

Ikumbukwe kuwa Kylian Mbappe mkataba wake na PSG utamalizika mwishoni mwa msimu huu n atayari alishakiri kutamani kuichezea klabu ya Real Madrid na almanusra ajiunge nayo miezi miwili iliyopita.

Mpaka sasa Mbappe ameshacheza michezo 12 kwenye Ligue 1 na michuano ya klabu bingwa ulaya, amefunga mabao 5 na kutengeneza assist 7 hivyo kuhusika kwenye mabao 17 katika michezo 10.