Katibu mkuu Yanga, Charles Boniface Mkwasa
Mkwasa amebainisha hayo katika taarifa aliyoitoa leo kwa kusema walipanga kucheza mechi moja katika uwanja wa Jamhuri uliopo Dodoma, lakini imeshindikana hivyo wataamishia mchezo huo katika jiji la Arusha.
"Tumeweka mipango yetu vizuri tutalipeleka kombe letu Dodoma ili wanachama wetu na wabunge wenye mapenzi na Yanga SC walione kombe letu ambalo tumelichukua mara tatu mfululizo. Tulipanga kucheza mechi moja Dodoma lakini uwanja umefungwa hivyo tutawaonesha na kuondoka kuelekea jijini Arusha....Ukiachilia mbali mikoa hiyo miwili msafara wa Yanga utajitahidi popote unapokatisha kusimama kidogo kuwaonesha wanachama wake kombe lao ili kufurahia juhudi na kazi". Alisema Mkwasa
Yanga inatarajia kucheza mchezo huo wa kirafiki mwishoni mwa juma hili.