Alhamisi , 17th Sep , 2020

Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC leo inaondoka kuelekea Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kucheza mchezo wao watatu dhidi ya Mwadui FC ya Mkoani humo.

Wachezajin wa KMC FC wakiwa mazoezini uwanja wa Uhuru Dar es salaam

KMC inakwenda kucheza mchezo wake wa kwanza kwa mechi ya ugenini na kwamba inajipanga katika kuhakikisha kuwa inafanya vizuri katika mchezo huo kama ilivyokuwa katika michezo miwili iliyopigwa katika Dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo ambayo hivi sasa inaongoza ligi, mbali na mchezo huo wa Mwadui FC lakini pia itacheza mchezo mwingine na Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera Septemba 25 mwaka huu.

Timu ya KMC FC katika msafara huo, itaondoka na wachezaji 22 huku wachezaji sita wakiachwa akiwemo Sadalla Mohamed Lipangile ambaye ni majeruhi lakini Afya yake ikiwa inaendelea kuimarika vizuri.

KMC inakwenda kukutana na Mwadui katika uwanja wa Mwadui Complex na kwamba inatarajia kuwasili mkoani humo Septemba 19 na na hivyo itapumzika kabla ya kuanza kwa mazoezi mengine ya kujiweka tayari dhidi ya mchezo huo.

Katika michezo yake miwili ya nyumba, KMC FC ilifanya vizuri kwa kuanza kuifunga Mbeya City Magoli manne kwa sifuri, Tanzania Prisons magoli mawili kwa moja na hivyo kuiwezesha kusalia katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.