Kisa na mkasa kufungiwa kwa Daniel Wanjiru

Alhamisi , 15th Oct , 2020

Wanjiru afungiwa kwa miaka 4 Mwanariadha Daniel Wanjiru wa Kenya, ambaye ni mshindi wa Marathon ya London 2017, amepigwa marufuku kushiriki mashindano yoyote ya riadha hadi mwaka 2023 kwa kutumia dawa zilizozuiwa michezoni.

Mwanariadha wa Kenya, Daniel Wanjiru(Pichani).

Wanjiru alisimamishwa kwa muda mnamo Aprili mwaka huulakini alikanusha kuchukua dawa iliyokatazwa na akaomba mahakama kubatilisha uamuzi huo.

Kitengo cha maadili kutoka Shirikisho la riadha kimethibitisha marufuku ya mtu mwanamichezo huyo mwenye umri wa miaka 28, na sasa atakaa nje ya uwanja hadi tarehe 8 Desemba, 2023.

Maelezo yaliyochapishwa zimearifu kwamba Wanjiru alirudisha sampuli inayoonyesha viwango vya seli nyekundu za damu ambazo hazikuwa na "maelezo ya kisaikolojia". Alijaribiwa mara 16 kati ya Aprili 2017 na 2019.

Katika majaribio hayo ya tarehe 14 na 9 Machi 2019 , alionyesha viwango vya juu vya mkusanyiko wa hemoglobin. Ilihitimishwa kuwa mabadiliko ya viwango kati ya majaribio hayawezi kuelezewa na sababu nyingine yoyote isipokuwa udanganyifu wa damu".

Wanjiru alishinda Marathon ya Amsterdam ya 2016 na alimaliza nafasi ya 8 na ya 11 kwenye mbio za London mnamo 2018 na 2019 mfululizo.