Jumatatu , 28th Sep , 2020

Mlinzi wa Benfica, Ruben Dias atajiunga na Man City kwa ada ya uhamisho wa paundi za kiingereza milion 65.

Ruben Dias beki wa kati wa Benefica anayetajwa kujiunga Man City

City wamelazimika kwenda sokoni kutafuta beki wa kati, baada ya matokeo mabovu ya kufungwa 5-2 na leicester city jumapili hii

“ Nalazimika kutafuta beki wa kiwango cha kimataifa ili kuimarisha safu ya ulinzi, kipigo hichi ni kikubwa na kinafichua udhaifu uliopo kwenye safu yangu ya ulinzi, sikutegemea wala sikuwahi kufikiri kuna siku nitafungwa kwa idadi hii' alisema kocha Pep Guardiola

Katika hali ya kushangaza beki wa kati wa Man City Nicolas Otamendi anatajwa kwenda kujiunga na benefica kwa ada ya paundi milion 13.7 kuziba pengo la Ruben Dias anayekwenda City biashara hizi hazijahusisha mabadilishano kila moja imejitegemea

Safu ya ulinzi ya Man City inayoongozwa na Otamedi imekuwa na mapungufu kadhaa ya kiuchezaji na majeruhi ya mara kwa mara ya mchezaji kama Aymaric Laporte imechangia kutokuwa na safu bora ya ulinzi, Guardiola alilazimika kumsajili Nathan Ake kutoka bournemouth ambaye bado hajakidhi mahitaji ya halisi ya ulinzi

Katika msimu huu City imeruhusu magoli 6 katika michezo miwili tu, katika mchezo wa kwanza dhidi ya Wolves uliomalizika kwa ushindi wa City 3-1 na mchezo wa pili waliopoteza kwa bao 5-2 dhidi ya leicester.

Matokeo haya yanaleta mashaka kuipita rekodi yao ya mwaka jana ambayo katika michezo 38 walifungwa magoli 35 na wao kufunga magoli 102.