Ijumaa , 15th Jul , 2022

Kocha wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Kim Poulsen amesema anahitaji ushindi kwenye mechi zao dhidi ya Somalia ili kusonga mbele zaidi kwenye hatua ya kufuzu Fainali ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Kocha wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Kim Poulsen

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika makao makuu ya shirikisho la mpira wa miguu ,TFF  Kim amesema wanatakiwa washinde mechi za raundi ya kwanza ili wajiweke kwenye mguu wa kufuzu katika fainali hizo.

“Tukishinda mechi hii tutakuwa tupo sehemu nzuri ya kufuzu kwenye Fainali hizi, wachezaji ni sehemu nzuri kwao kama tukifuzu,” amesema Kim.

Stars itacheza mchezo wake wa kwanza Julai 23 na marudiano 30 Julai na mechi zote zikichezwa katika uwanja wa Mkapa huku Fainali za CHAN zinatarajia kufanyika Januari mpaka Februari 2023 nchini Algeria.