Jumamosi , 22nd Apr , 2017

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara Young Africans leo wanashuka dimbani kuvaana na Tanzania Prisons FC katika hatua ya robo fainali ya nne ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dsm

Kikosi cha Yanga

Hata hivyo uongozi wa timu ya Yanga umeweka hadharani kikosi chake cha maangamizi dhidi ya Wajelajela huku wakijitapa kutumia mfumo wa 4-4-2,

Kikosi hicho ni kama ifuatavyo;
1. Beno Kakolanya 
2. Hassani Kessy
3. Haji Mwinyi 
4. Kelvin Yondani
5. Nadir Haroub 
6. Juma Makapu
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Obrey Chirwa
10. Amisi Tambwe
11. Geofrey Mwashuiya

Akiba -

-Deogratius Munishi
- Oscar Joshua - Andrew Vicent - Juma Mahadhi
- Antony Matheo
- Yusufu Mhiru
- Emanuel Martin 

Kwa upande mwingine, timu itakayoibuka na ushindi siku ya leo itaweza kuungana na timu nyingine tatu ambazo tayari zimefuzu kwa hatua ya Nusu Fainali ambazo ni Mbao FC, Simba SC pamoja na Azam FC.