Jumanne , 24th Mei , 2022

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania cha Wanawake chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Girls kimerejea nchini kikitokea nchini Cameroon ambako kilicheza mchezo wa raundi ya 4 wakuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Cameroon na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Kikosi cha Serengeti Girls kikiwa Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume visiwani Zanzibar

Serengeti Girls wanarejea nchini baada ya kucheza mchezo wa mkndo wa kwanza wa raundi ya 4 ambayo ni ya mwisho kwenye michezo ya kuwania kufuzu kumbe la Dunia kwa wasichana chini ya umri huo. Mchezo uliochezwa Mei 22, 2022 Younde Cameroon.

Kikosi hicho kimetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume visiwani Zanzibar. Na mchezo wa mkondo wa pili watacheza katika uwanja wa Amani Zanzibar Juni 06, 2022. Ambapo mshindi wa jumla wa mchezo huu atafaku kucheza fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini India kuanzia Oktoba 11 hadi 30, 2022.