Jumatatu , 21st Sep , 2020

Kocha wa Klabu ya Mbeya City , Amri Said amesema wachezaji wake walishindwa kutumia nafasi walizotengeneza dhidi ya Azam hali iliyosababisha wapoteze mechi ya jana.

Kocha wa Mbeya City,Amri Said akizungumza an waandishi wa habari .

Mbeya City ilifungwa na Azam bao 1-0 lililofungwa na kiungo wa Rwanda, Ally Niyonzima dakika ya 25 ya mchezo, na kupelekea wana komakumwanya kufungwa mechi ya tatu mfululizo.

Akizungumzia kipigo hiko koha huyo wa zamani wa Lipuli, Mbao, na Biashara amesema anafanya kazi ya ziada ili Timu hiyo ipate matokea ya ushindi haraka iwezekanavyo.

''Timu inajitahidi kucheza, bahati mbaya wachezaji wangu hawakuzitumia nafasi tulizopata, sisi tukafanya kosa moja tukaadhibiwa,ndio mpira wa miguu ulivyo''

Katika mchezo wa kwanza, Mbeya City ilinyukwa bao 4-0, kabla ya kulala kwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City na jana ilibwangwa na Azam.

Upo uwezekano mkubwa Kocha, Amri Said akatupiwa virago iwapo Mbeya City itafungwa katika mechi mbili zijazo dhidi ya Tanzania Prisons na Namungo.

TAKWIMU ZA MBEYA CITY MSIMU HUU

Mechi 3

Ushindi-0

Kufungwa-3

Mabao ya kufunga-0

Mabao ya kufungwa-6

Alama ilizonazo-0