Kepa ataigharimu Chelsea,Takwimu zake majanga

Jumanne , 15th Sep , 2020

Nyota wa zamani wa Manchester United na Klabu ya Timu ya Taifa ya England,Garry Neville amesema mlinda mlango wa Chelsea Kepa Arrizabalaga hamfurahishi kocha wake Frank Lampard kufuatia kufungwa mabao mengi nje ya eneo lake.

Mlinda mlango wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga (Pichani) analaumiwa kwa kushindwa kuokoa michomo ya mbali.

Kepa alifungwa bao la nje ya eneo la penati lililofungwa na Leandro Trossard kwa mkwaju wa mbali dakika ya 54 na kuifanya Brighton kurejea mchezoni baada ya Chelsea kutangulia kwa bao la Jorginho aliyefunga kwa penati dakika ya 23 baada ya Timo Werner kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Ingawa Chelsea ilifunga mabao mengine mawili kupitia mlinzi wake wa kulia Reece James dakika ya 56 na Kurt Zouma dakika ya 66,bado Neville amedai kuwa Timu yoyote inayohitaji ubingwa inapaswa kuwa na mlinda mlango makini asiyefanya makosa ya mara kwa mara.

Neville ameongeza kuwa inawezekana Lampard anajaribu kutomzungumzia vibaya Kepa kwenye jumuiya ya watu lakini ukweli ni kwamba ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo lazima ataonyesha hasira dhidi ya mlinda mlango huyo aliyenunuliwa kwa pauni milioni 70 akitokea Athletic Bilbao.

Ameongeza kuwa tatizo lililopo kwa sasa Chelsea ni sawa

KEPA NDIYE KINARA WA KUFUNGWA MABAO YA MBALI 2019/20

Mlinda mlango huyu raia wa Hispania ameshika nafasi ya kwanza kwa kuruhusu mabao ya nje ya (Box) kwa msimu uliopita.

1-Kepa Arrizabalaga-19

2-Mat Ryan-18 (Brighton&Hove Albion

3-Martin Dubravka-14 (Newcastle United

4-Neil Etheridge-14 (Cardif City)

5-Jordan Pickford-14 (Everton)