Jumapili , 24th Sep , 2017

Juventus na Napoli zimekuwa klabu za kwanza kushinda michezo 6 mfululizo ya kwanza katika historia ya ligi kuu ya Italia Serie A.

Juventus wakiwa nyumbani jana waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Torino na kujiwekea rekodi ya kushinda michezo 6 ya mwanzo. Mabao ya Juventus yalifungwa na Paul Dybala (2) huku Miralem Pjanic na Alex Sandro wakifunga mengine.

Kwa upande wa Napoli nao hawakuwa nyuma wakiwa ugenini dhidi ya SPAL walishinda mabao 3-2 na kufikisha mechi 6 bila kupoteza hivyo kuwa sawa na Juventus.

Napoli wanaongoza msimamo wa Serie A wakiwa na alama 18 sawa na Juventus wakitofautishwa na idadi ya mabao ya kufungwa na kufunga. Wiki ijayo Juventus watakuwa ugenini dhidi ya Atlanta wakati Napoli atakuwa nyumbani dhidi ya Cagliari.