Jumapili , 28th Mei , 2017

Kiungo na Nahodha wa timu ya Simba SC, Jonas Mkude amepata ajali baada ya gari waliokuwa wakisafiri nalo kupinduka katika eneo laDumila Mkoani Morogoro wakati wakirejea jijini Dar es salaam kutokea Dodoma.

Jonas Mkude

Ajali hiyo iliyohusisha  gari yenye namba za usajili T 834 BLZ, Toyota VX imetokea baada ya gurudumu la nyuma ya gari hiyo kupasuka na kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Shose na majeruhi kadhaa ambapo wamewahishwa kwenye hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupatiwa matibabu.