Alhamisi , 26th Mei , 2022

Jaylen Brown na Jason Tatum waiongoza Boston Celtics kushinda mchezo wa 3 wa fainali ya NBA kanda ya mashariki kwa kuifunga Miami Heat kwa alama 93 kwa 80 kwenye mchezo wa 5 kati ya michezo 7 ya fainali.

Jaylen Brown amefunga alama 25 amechukua Rebound 4

Katika mchezo huu Jaylen Brown amefunga alama 25 amechukua Rebound 4 na pasi za kufunga (Assist) 1 na Jason Tatum amefunga points 22 Rebound 12 na pasi za kufunga (Assist) 9 na kuisaidia Celtcs kushinda na kuongoza Series kwa 3-2.

Kwa matokeo haya Boston Celtics wanahitaji ushindi kwenye mchezo unaofata wa 6 (game 6) utakaochezwa kesho Mei 27, ili kuwa mabingwa wa Mashariki na kufuzu fainali ya NBA msimu huu.