Jumapili , 7th Mar , 2021

Kuelekea mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya wenyeji Polisi Tanzania dhidi ya wageni wao Yanga SC kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Afisa Muhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema wapo tayari.

Afisa Muhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz

''Twende tukawape sapoti wachezaji wetu kwenye mchezo wa leo ili tupate alama 3 muhimu, iwe mvua iwe jua leo atoki mtu'', amesema Nugaz.

Nugaz ameongeza kuwa kocha mkuu wa timu hiyo Cedric Kaze amesema kuwa amewaadaa wachezaji wote hivyo kila atakayechaguliwa kuanza leo atakuwa tayari kuzisaka pointi tatu.

Yanga SC ndio vinara wa ligi kuu wakiwa na pointi 49 katika mechi 22, mbele ya Simba SC yenye pointi 45 katika mechi 19.

Kwa upande wa Polisi Tanzania inashika nafasi ya 8 ikiwa na pointi 28, itakuwa inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi dhidi ya KMC kwenye mchezo uliopita.