Hivi ndivyo tutakavyoifunga Simba - Azam FC

Thursday , 12th Jan , 2017

Kuelekea fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kesho Ijumaa, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, ameweka wazi kuwa wanajua namna ya kuikabili Simba na kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

Azam wakiwa mazoezini

Cheche ametoa kauli hiyo kwenye mazoezi ya kwanza ya Azam FC kujiandaa na mchezo huo, ambapo imeingia fainali baada ya kuichapa Taifa Jang’ombe bao 1-0, lililofungwa kwa shuti kali na kiungo Frank Domayo.

“Mchezo utakuwa mgumu, sisi tumewaona tokea mwanzo kwenye michuano hii na tunawajua tokea huko nyuma na mwalimu waliokuwa naye na sisi tulikuwa naye tunamjua na tunajua ni vitu gani tutafanya, hatuwezi kusema hivi sasa utakuja kuviona uwanjani wakati tunacheza kama tulivyowaahidia kwenye mechi na Yanga,” alisema Cheche

Cheche ambaye atakiongoza kikosi hicho kama kocha mkuu hadi kumalizika kwa michuano hiyo kabla ya kumpisha Kocha Mkuu mpya wa Azam FC aliyetambulishwa jana, Aristica Cioaba raia wa Romania, mpaka sasa amekiongoza kikosi hicho kuandika rekodi ya aina yake ya kutofungwa mchezo wowote wala kuruhusu bao.

Hadi inaingia fainali kwa kuitoa Taifa ya Jang’ombe, Azam FC kwenye hatua ya makundi iliichapa Zimamoto bao 1-0, ikatoa suluhu na Jamhuri kabla ya kuifumua Yanga mabao 4-0, ukiwa ni ushindi wa kihistoria tokea timu hizo zianze kukutana.

Timu hiyo leo jioni itamalizia mazoezi yake ya mwisho kabla ya kuivaa Simba kwenye mchezo wa fainali unaosubiriwa kwa hamu na mamilioni ya Watanzania wapenzi wa soka.

Recent Posts

Rais Magufuli

Current Affairs
Rais Magufuli amteua Prof. Chibunda

Muigizaji mkongwe nchini Jacob Stephen 'JB '

Entertainment
Wasanii wasiopiga kelele hawategemei filamu - JB

Msajili wa vyama siasa, Jaji Francis Mutungi.

Current Affairs
Msajili wa vyama vya siasa alaani vurugu za CUF