Jumamosi , 17th Apr , 2021

Mshambualiaji na nahodha wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Harry Kane ameonesha kiwang o safi kwa kufunga mabao mawili yalioisaidia timu yake kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Everton usiku wa jana ugenini kwenye dimba la Godison park.

Mshambuliai Harry Kane, akionekana kwenye matukio tofauti tofauti.

Mabao hayo yamemfanya Harry Kane kufikisha maba0 21 na kuongoza orodha ya wafumania nyavu kwenye ligi kuu England mpaka sasa kwa msimu huu akifuatiwa na mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah mwenye mabao 19.

Kane pia amefikisha mabao 164 na kuwa mshambuliaji wa saba mwenye mabao mengi wa muda wote kwenye historia ya ligi hiyo ambayo inaongozwa na mshambuliaji wa zamani na Newcastle na timu ya taifa ya England, Alan Shearer mwenye mabao 260.

Baada ya kuonesha umahiri wa kupachika mabao na kuweka rekodi nyingine ya kufunga mabao kuanzia 20 na kuendelea kwa misimu mitano mfululizo, lakini nyota huyo alifanyiwa mabadiliko dakika ya 90+3 baada ya kupata maumivu ya kifundo cha mguu na Delle Alli kuingia.

Utata uliosalia ni kwamba, bado hajajulikana nyota huyo ameumia kwa kiasi gani na lini atarejea uwanjani ambo linalomuumiza kichwa kocha wake Jose Mourinho kwani nyota huyo ndiye hodari wa kutengeneza mabao, mabao 16 kwenye ligi hiyo.