Jumatatu , 25th Sep , 2017

Nahodha wa West Ham United Mark Noble amesema mshambuliaji wa Tottenham Hospurs Harry Kane ana thamani ya zaidi ya Pauni milioni 100 sawa na Bilioni 303,791,000,000 za Kitanzania.

Noble amesema uwezo wa Harry Kane ni mkubwa sana na ndio mshambuliaji bora duniani kwasasa hivyo thamani yake ni kubwa zaidi.

“Ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, ni mshambuliaji bora duniani, anastahili kuuzwa kwa zaidi ya Pauni milioni 100 (Tsh. 303,791,000,000) Bilioni  kama ilivyokuwa kwa Gareth Bale”, alisema Noble kwenye mahojiano na Wanahabari.

Harry Kane alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa 3-2 iliopata Tottenham dhidi ya West Ham siku ya Jumamosi. Kane sasa amefunga mabao 6 katika michezo 7 msimu huu.