Jumanne , 26th Sep , 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema anamtaka mkandarasi atakayeshughulikia uwanja wa taifa aweze kutoa tiketi zenye kuonesha namba siti ambayo mtu ataenda kukaa moja kwa moja na siyo masuala ya ubabaishaji.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe ametoa kauli hiyo wakati alipoenda kutembelea uwanja wa mpira wa miguu wa Nangwanda uliopo Mkoani Mtwara na kusema anahitaji mabadiliko katika viwanja vyote vya michezo ili viweze kuwa bora zaidi na kufanana na viwanja vingine vilivyopo duniani.

"Namtegemea mkandarasi anayekuja katika uwanja wa Taifa, na hili nitaeleza mpaka mwisho atuletee mabadiliko ambayo tunayataka na nitasisitizia hilo. Atakayetoa tiketi kwa namba za viti, siyo holela watu wanakaa sehemu za kutembelea kwa miguu. Maana sasa huelewi wameingia watu wangapi ?, ni lini Watanzania tutaweza kutendea haki hata viwanja vyetu vya kisasa. Kiwanja kipya kitakachokuja baada ya ukarabati, kitakachotokea pale ", amesema Dkt. Mwakyembe.

Mtazame hapa chini Dkt. Mwakyembe akiongelea zaidi kuhusu viwanja vya kimichezo vilivyopo chini Tanzania.