Jumatano , 25th Nov , 2020

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba SC Mohammed Dewji  na Mbunge wa Nzega Vijijini Hamis Kigwangalla, wamemaliza tofauti zao.

Kushoto ni wachezaji wa Simba SC na kulia ni Mohammed Dewji na Hamisi Kigwandalla

Mo Dewji ameweka wazi hilo leo Novemba, 25, 2020 kwa kuomba radhi kwa pale alipomkosea Kigwangalla wakati wakijibizana juu ya Bilioni 20 za uwekezaji Simba. Lakini pia ameweka wazi kuwa ameshasamehe kwa pale alipokosewa na Kigwangalla, huku akieleza nia ilikuwa ni kuijenga Simba SC.

Hivi Karibuni Kigwangalla pia aliweka wazi kuhusu kumaliza tofauti hizo na kueleza kuwa yeye ameshasamehe na sasa washirikiane kujenga klabu.