Jumatatu , 20th Feb , 2017

Nyota wa timu ya Pelicans, Anthony Davis mwenye umri wa miaka 23, ameweka rekodi ya kufunga pointi 52 na kuisaidia timu yake ya upande wa Magharibi kupata ushindiwa pointi 192 kwa 182 dhidi ya timu ya Mashariki katika mchezo maalum alfajiri ya leo.

Anthony Davis

Awali Davis aliweka wazi kabla ya mchezo huo maalum wa NBA, maarufu kama All-Star Game usiku wa kuamkia leo, kuwa alipania kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo, maarufu kama MVP, ahadi ambayo ilitimia

Nyota huyo wa Pelicans amefanikiwa kuvunja rekodi ya ufungaji ya mchezo huo ya pointi 42 iliyowekwa na Wilt Chamberlain mwaka 1962.

Mchezo wa NBA All-Stars huchezwa kila mwaka kati ya sehemu ya Magharibi na sehemu ya Mashariki mwa nchini Marekani na mwaka huu, mchezo huo ulichezwa katika Uwanja wa Smoothie King ambao ni uwanja wa nyumbani wa timu ya Pelicans.