Jumatano , 20th Oct , 2021

Mabingwa watetezi wa ligi ya Kikapu nchini Marekani ‘NBA’, Milwaukee Bucks imeanza vema kampeni ya kutetea ubingwa wake kwa kuifunga Brooklyn Nets kwa alama 127-104 kwenye mchezo wake wa ufunguzi wa msimu mpya wa NBA 2021-22

(Picha ikionesha matukio mbalimbali kwenye michezo ya ugunguzi ya NBA.)

Kwenye mchezo huo uliochezwa saa 8:30 usiku wa leo Oktoba 20, 2021, Bucks waliendelea kujivunia ubora wa nyota wake Giannis Antetokounmpo aliyekuwa kinara wa mchezo kwa kufikisha alama 32, rebound 14 na Assist 7.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwana kwa Brooklyn Kucheza bila Kyrie Irving ambaye yupo nje ya timu kwasbabu ya kugomea kuchanja chanjo ya Covid-19 wakati Kocha wa Bucks, Budenholzer amthibitisha kuwa Jrue Holiday yupo fiti licha ya kushindwa kumaliza mchezo na kutolewa kwenye Quater ya pili akisumbuliwa na maumivu ya kisigino.

Kwa upande mwingine, Mabingwa mara 17 wa NBA, Wakongwe Los Angeles Lakers wameangukia pua baada ya kufungwa kwa alama 121-114 dhidi ya Golden State Warriros licha ya lakers kuongoza Quarter 3 na kupinduliwa meza mwishoni.

Licha ya kupoteza mchezo huo, Lakini nyota wa Lakers, Lebron James ameibuka kuwa nyota wa mchezo kwa kukusanya alama 34, rebound 11 na Assist 5 ambazo pia hazikutosha kubeba Lakers ibadili matokeo.

Nyota Golden State Warriros, Stephen Curry alionesha kiwango kizuri kwa kukusanya alama 21, rebound 10 na Assist 10 ambazo walishirikiana vema na Bjelica Nemanja alama 15, rebound 11 na Assist 4 ambazo zilichangia ushindi wa Golden.

Kipigo hicho ni cha saba mfululizo kwa Lakers tokea kuanza kwa michezo ya NBA Pre-Season ambapo walicheza michezo 6 na kufungwa yote. Walifungwa mara mbili na Golden State hivyo kipigo cha alfajiri ya leo ni cha tatu mfululizo kwa Lakers.

NBA itaendelea tena usiku wa kuamkia kesho kwa michezo 11, lakini baadhi ya michezo inayosubiriwa kwa hamu ni ule utakaowakutanisha Makamu bingwa, Phoenix Suns dhidi ya Denver Nuggets na Memphis Glizzlies na Cleveland Cavaliers.