Jumanne , 25th Jan , 2022

Nahodha wa timu John Bocco, amesema hatuna presha ya kurejea kileleni mwa msimamo ingawa amekiri ligi ya msimu huu ni ngumu.

(Nahodha wa Simba SC, John Rafael Bocco)

Bocco amesema timu yao inapambana kuhakikisha wanarudi kileleni mwa msimamo licha ya ugumu huo ambapo kila kitu kinaenda sawa na malengo hayo yatafikiwa hivi karibuni.

Bocco amesema hayo wakati akizungumzia mchezo wao ujao wa kiporo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar  utakaopigwa Januari 26  Uwanja wa Kaitaba nakusema  kuwa utakuwa mgumu lakini watahakikisha wamapata ushindi .

“Kagera Sugar  ni timu bora tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini kwa maandalizi waliyofanya  wanaamini wataibuka na ushindi licha ya hivi karibuni kutokuwa na matokeo mazuri katika baadhi ya michezo waliocheza. Lakini tutafuata maelekezo tutakayopewa na mwalimu na tunaamini tutafanikiwa,” amesema Bocco.

Kikosi cha Simba  kimeondoka   asubuhi kuelekea mkoani Kagera tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya wenyeji Kagera Sugar utakaopigwa Jumatano Uwanja wa Kaitaba.