Jumamosi , 26th Sep , 2020

Kocha wa Real Madrid mfaransa Zinedine Zidane anaamini FC Barcelona inakikosishindani kinachoweza kuwania mataji msimu huu licha ya changamoto wanazopitia.

Zinedine Zidane alikiongoza kikosi cha Real Madrid kutwaa ubingwa wa La Liga msimu uliopita kwa tofauti ya alama tano dhidi ya FC Barcelona

Msimu uliopita FC Barcelona walimaliza msimu mikono mitupu kwani hawakushinda taji lolote na ilikuwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka kumi na mbili kumaliza msimu pasipo kushinda taji, mara ya mwisho Barcelona kumaliza msimu bila kushinda taji ilikuwa msimu wa 2007-08.

Licha ya msimu uliopita kutokuwa mzuri kwa FC Barcelona ambayo pia imekuwa na migogoro katika uongozi wake lakini kocha wa mahasimu wao Real Madrid Zidane amesema

"Nadhani kila klabu ina mambo yake na shida zake. Nadhani Barcelona ​​kwa upande wa timu na kikosi, ni klabu ambayo inaweza kupigania kushinda kila kitu”

Barcelona wameanza ujenzi wa timu mpya chini ya kocha Ronald Koeman na tayari wachezaji kadhaa wameondolewa kwenye kikosi ikiwa ni katika harakati za kujenga timu yenye sura mpya wachezaji walioondoka ni mshambulliaji Luis Suarez, viungo Arturo Vidal, Ivan Rakitic, Arthur na mlinzi Nelson Semedo.

wakati mchezaji Philippe Coutinho amerejeshwa kwenye kikosi akitokea Bayern Munich ambako alicheza kwa mkopo msimu uliopita, lakini pia wamemsajili kiungo Miralem Pjanic kutoka Juventus ya Italia.

Wakati kocha Zidane kikosi chake cha Real Madrid hakijabadilika sana kimekuwa na mabadiliko machache kwani mchezaji pekee aliyeongezeka kwenye kikosi hicho ni Martin Odegaard ambaye amerejea kutoka Real Sociedad ambako alikuwa kwa mkopo msimu uliopita, na wachezaji waliotoka ni Gareth Bale aliyejiunga na Tottenham kwa mkopo wa msimu mzima, Alvaro Morata nae kajiunga na Juventus kwa mkopo na James Rodriguez ameuzwa, amejiunnga na Everton.

Msimu uliopita Real Madrid walichukua ubingwa wa La Liga kwa tofauti ya alama tano dhidi ya Barcelona ambao walimaliza nafasi ya pili.

Barcelona watacheza mchezo wao wa kwanza wa Ligi kuu Hispania La Liga msimu wa 2020-21 dhidi ya Villarreal kesho Jumapili, wakati Real Madrid wao wanashuka dimba Leo Usiku dhidi ya Real Betis.