Jumatano , 18th Jan , 2017

Beki wa kimataifa wa Zimbambwe na Klabu ya Simba Method Mwanjali amejishinda tuzo ya mchezaji bora wa klabu ya Simba kwa mwezi wa 12 mwaka jana 2016

Method Mwanjali

Mashabiki wa klabu hiyo wameonesha kufurahishwa sana na uwezo na jitihada za mchezaji huo alizozionesha mwaka jana na katika kipindi cha michuano ya kombe la Mapinduzi yaliyofanyika Zanzibar.

Haya ni baadhi ya maoni mbalimbali ya mashabiki wa Simba juu ya ushindi wa mchezaji bora wa mwezi wa 12 alioupata Method Mwanjali 

Edina Chuma: Nimeipenda ndiyo maana akaitwa baba mwenye nyuma, amenipa raha sana Zenji hongera Mwanjali tunaomba kesho (Leo) mtupe raha MOro maana hawa wamesha bakiza point moja inabidi muwaongezee mtaji wazid kusota"

Mwimbileghe Petro Mwaigaga: Ulistahili kabisa hii tuzo lakini Zimbabwe wameshindwa kukuona ukaitumikie timu yako ya taifa!! kama vipi badili uraia uwe Mtanzania maana bongo hakuna beki wa kati kama wewe Mwanjali.

Haya ni maoni ya baadhi yao