Jumanne , 17th Jan , 2017

Ligi kuu ya Soka Tanzania bara inaendelea Jumatano ambapo vinara wa Ligi Simba SC watakuwa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro huku Azam FC ikiahidi kuendeleza ubabe wake kwa Mbeya City Uwanja wa Chamazi Dar es salaam.

Kikosi cha Azam kikishangilia ubingwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi

Afisa habari wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema, mchezo wa kesho anaamini utakuwa ni mgumu lakini kila kitu ni maandalizi na wamejipanga kwa ajili ya kukabiliana na changamoto katika mchezo huo ili kuhakikisha wanapata ushindi wa nyumbani hapo kesho.

Jaffary amesema mpaka sasa hakuna majeruhi katika kikosi na wanachosubiri kwa sasa ni mchezo huo wakiamini watafanya vizuri kwani wameweza kuzifunga timu kongwe za Simba na Yanga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi lililofanyika visiwani Zanzibar.

Jaffary amesema, Kocha Iddy Cheche ataendelea kuwa katika benchi la ufundi mpaka pale vibali vya kocha mpya wa Azam FC Mromania Aristica Cioaba vitakapokamilika.

Dismas Ten - Msemaji wa Mbeya City

Kwa upande wake kocha msaidizi wa Mbeya City Josia Steven amesema, anaamini Azam FC ni kikosi kizuri na wanachangamoto kubwa ya kukabiliana nao lakini wamejipanga vizuri zaidi hivyo Azam FC wasitegemee kuwafunga kama walivyofanya kwa Simba na Yanga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi lililofanyika visiwani Zanzibar.

Msikilize hapa Msemaji wa Mbeya City, Dismas Ten