Jumanne , 14th Feb , 2017

Baada ya mapumziko ya siku moja kikosi cha Azam FC kimeendelea na mazoezi, katika kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Red Arrows ya Zambia, siku ya Jumatano kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Wachezaji wa Azam FC wakijifua

Mbali na mechi hiyo ya kimataifa, pia Azam inajiwinda na mchezo wa wake wa ligi kuu dhidi ya Mwadui FC mwishoni mwa wiki, mechi zote zikianza saa 1:00 usiku.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema wamekubali mchezo huo kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa raundi ya kwanza wa michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya mshindi wa jumla kati ya timu za Orapa United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Tayari timu ya Red Arrows imeshawasili Dar es Salaam, kujiandaa na mchezo huo na wao hiyo inakuwa ni maandalizi ya msimu mpya wa Ligi ya Zambia ambayo inatarajia kuanza siku za karibuni.