Azam FC waaga mashindano

Sunday , 19th Mar , 2017

Klabu ya Azam ya Jijini Dar es Salaam, imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Mbabane Swallows ya Swaziland.

Azam Vs Mbabane Swallows, Chamazi DSM.

Katika mchezo huo wa marudiano uliopigwa katika Jiji la Mbabane nchini Swaziland, Mbabane Swallows walianza kupata bao la kwanza katika dakika ya 41 ya mchezo, huku mengine mawili yakipatikana katika kipindi cha pili.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Jumapili iliyopita katika dimba la Chamazi Dar es Salaam, Azam walipata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Ramadhan Singano, na sasa kwa matokeo haya, Azam wanakuwa wametupwa nje kwa jumla ya mabao 3-1.

Licha ya matokeo hayo, Azam pia wamelalamikia kile walichodai ni vitendo vya kufanyiwa vurugu uwanjani, jambo ambalo linaweza kuwa limechangia matokeo ya aina hiyo.

Recent Posts

Msanii Beka Flavour

Entertainment
"Simuogopi wala simfikirii Aslay" - Beka Flavour

Matajili wa Alizeti timu ya soka ya Singida United ya Singida wakijifua jijini Mwanza.

Sport
Singida United yasajili 16

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Current Affairs
Tiba asili na tiba mbadala wabanwa

Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Current Affairs
Wabunge nane CUF wavuliwa Uanachama